Discuss with your friends

Would you like to discover for yourself what God is like and how God wants you to live?

Most people like to make these discoveries in a group with their friends. Here are some questions to get your discussion started


    

Discovering Spiritual Community #20

Caring for one another

1. Una shukuru kwa ajili ya nini juma hili?

2. Una sumbukana na nini na jinsi gani tunaweza kukusaidia?

Accountability

3. Ni vipi uliweka kwa matendo tulio jifunza mwisho?

4. Ulishiriki na nani somo lililopita na matokeo yalikuwaje?

5. What needs did you meet in the community last week?

Discover

6. Uliza mtu asome kifungo kimoja kwa wakati.

7. Kuwa na mmoja katika kikundi na aseme kifungo kwa maneno yake mwenyewe.

8. Uliza kikundi kama amewacha au kuongeza kitu.

Siku ya Jumapili, alfajiri na mapema, wale wanawake wali chukua yale manukato waliyokuwa wameyaandaa wakaenda kaburini.Wakakuta jiwe limeondolewa kwenye mlango wa kaburi.Lakini walipoingia ndani, hawakuona mwili wa Bwana Yesu.Walipokuwa wanashangaa juu ya jambo hilo, ghafla, watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayong’aa sana, wakasimama karibu nao.Wale wanawake, kwa hofu, wakainamisha nyuso zao chini. Lakini wale watu wakawaambia, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai mahali pa wafu?Hayuko hapa; amefufuka. Kumbukeni alivyowaambia alipokuwa Gali laya,kwamba ilikuwa lazima Mwana wa Adamu awekwe mikononi mwa watu waovu, asulubiwe na siku ya tatu afufuke.”Wakayakumbuka maneno ya Yesu.Waliporudi kutoka huko kaburini wakaeleza mambo haya kwa wale wanafunzi kumi na mmoja pamoja na wengine wote.10 Hao wanawake walikuwa ni Mariamu Magdalene, Yoana na Mariamu mama yake Yakobo pamoja na wengine waliofuatana nao.11 Maelezo yao yalionekana kama upuuzi kwa hiyo hawakuwaamini.12 Bali Petro akaondoka mbio, akaenda kaburini. Alipoinama, akaiona ile sanda, ila hakuona kitu kingine zaidi. Akarudi nyumbani akis taajabia yaliyotokea.

Yesu Awatokea Wanafunzi Wawili

13 Siku hiyo hiyo, wanafunzi wawili wa Yesu walikuwa wanak wenda kijiji cha Emau, yapata maili saba kutoka Yerusalemu,14 nao walikuwa wakizungumzia mambo yote yaliyotokea.15 Wali pokuwa wakizungumza, Yesu mwenyewe alikuja akatembea pamoja nao,16 lakini wao hawakumtambua.17 Akawauliza, “Ni mambo gani haya mnayozungumzia wakati mnatembea?” Wakasimama , nyuso zao zikionyesha huzuni.18 Mmoja wao, aliyeitwa Kleopa, akamwambia, “Nadhani ni wewe tu katika watu wote wanaoishi Yerusalemu ambaye hufahamu mambo yaliyotokea siku hizi chache zilizopita.”

19 Akawauliza, “Mambo gani?” Wakamjibu “Mambo yaliyompata Yesu Mnazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo mkuu katika maneno yake na matendo yake, mbele za Mungu na mbele za wanadamu.20 Makuhani wakuu na viongozi wetu walimtoa ahukumiwe kufa na wakamsulubisha.21 Na sisi tulikuwa tumetegemea kwamba yeye ndiye angeliikomboa Israeli. Zaidi ya hayo leo ni siku ya tatu tangu mambo haya yatokee.22 Isitoshe, baadhi ya wanawake katika kundi letu wametushtua; walikwenda kaburini leo alfajiri23 lakini hawakuukuta mwili wake. Waliporudi walisema wamewaona malaika ambao waliwaambia kwamba Yesu yu hai.24 Baadhi yetu walikwenda kaburini wakakuta mambo ni kama walivyoelezea wale wanawake, ila yeye mwenyewe hawakumwona.”

25 Kisha Yesu akawaambia, “Ninyi ni watu wajinga. Mbona mnaona ugumu kuamini mambo yote yaliyosemwa na Manabii?26 Je, haikumpasa Kristo kuteswa na kwa njia hiyo aingie katika utukufu wake?”27 Akawafafanulia maandiko yalivyosema kumhusu yeye, akianzia na maandiko ya Musa na kupitia maandiko yote ya manabii.

28 Walipokaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, Yesu akawa kama anaendelea na safari.29 Lakini wakamsihi akae nao wakisema, “Kaa hapa nasi kwa maana sasa ni jioni na usiku unain gia.” Basi akaingia ndani kukaa nao.30 Alipokuwa nao mezani, akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akaanza kuwagawia.31 Ndipo macho yao yakafumbuliwa, wakamtambua! Lakini akatoweka, hawakumwona tena.

32 Wakaulizana, “Je, mioyo yetu haikuchangamka kwa furaha alipokuwa anazungumza nasi njiani na kutufafanulia Maandiko?”33 Wakaondoka mara moja, wakarudi Yerusalemu. Wakawakuta wale wanafunzi kumi na mmoja na wale waliokuwa pamoja nao, wamekusany ika34 wakisema, “Ni kweli Bwana amefufuka! Amemtokea Simoni.”35 Kisha wale wanafunzi wawili wakaeleza yaliyotokea njiani na jinsi walivyomtambua Yesu alipoumega mkate. Yesu Awatokea Wanafunzi Wake

Read full chapter