Discuss with your friends

Would you like to discover for yourself what God is like and how God wants you to live?

Most people like to make these discoveries in a group with their friends. Here are some questions to get your discussion started


    

Discovering Spiritual Community #19

Caring for one another

1. Una shukuru kwa ajili ya nini juma hili?

2. Una sumbukana na nini na jinsi gani tunaweza kukusaidia?

Accountability

3. Ni vipi uliweka kwa matendo tulio jifunza mwisho?

4. Ulishiriki na nani somo lililopita na matokeo yalikuwaje?

5. What needs did you meet in the community last week?

Discover

6. Uliza mtu asome kifungo kimoja kwa wakati.

7. Kuwa na mmoja katika kikundi na aseme kifungo kwa maneno yake mwenyewe.

8. Uliza kikundi kama amewacha au kuongeza kitu.

32 Wahalifu wengine wawili pia walipelekwa wakasulubiwe pamoja na Yesu.33 Walipofika mahali paitwapo “Fuvu la kichwa,” wakamsulubisha Yesu hapo pamoja na hao wahalifu; mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto.

34 Yesu akasema, “Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui wali tendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura.35 Watu wakasi mama pale wakimwangalia. Viongozi wa Wayahudi wakamdhihaki wakisema, “Si aliokoa wengine! Ajiokoe mwenyewe basi, kama kweli yeye ndiye Kristo wa Mungu, Mteule wake.”36 Askari nao wakam wendea, wakamdhihaki. Wakamletea siki anywe,37 wakamwambia, “Kama wewe ni mfalme wa Wayahudi, jiokoe tuone.”

38 Na maandishi haya yaliwekwa kwenye msalaba juu ya kichwa chake: “HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI.”39 Mmoja kati ya wale wahalifu waliosulubiwa naye akamtu kana, akasema: “Wewe si ndiye Kristo? Jiokoe na utuokoe na sisi.”

40 Yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akisema, “Wewe humwogopi hata Mungu! Wote tumehukumiwa adhabu sawa.41 Adhabu yetu ni ya haki kwa sababu tunaadhibiwa kwa makosa tuliyofanya. Lakini huyu hakufanya kosa lo lote.”42 Kisha akasema, “Bwana Yesu unikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.”43 Yesu akam jibu, “Nakuambia kweli, leo hii utakuwa pamoja nami peponi.”

Yesu Afa Msalabani

44 Ilikuwa kama saa sita mchana. Kukawa na giza nchi nzima mpaka saa tisa,45 kwa maana jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likapasuka katikati kukawa na vipande viwili.46 Yesu akapaza sauti akasema, “Baba, mikononi mwako ninaikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.

47 Mkuu wa maaskari alipoona yaliyotokea, akamsifu Mungu akasema, “Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.”48 Na watu wote waliokuwa wamekusanyika hapo kushuhudia tukio hilo walipoy aona hayo, walirudi makwao wakijipiga vifua kwa huzuni.

49 Lakini wale wote waliomfahamu, pamoja na wanawake wal iokuwa wamemfuata kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiyata zama mambo haya. Yesu Azikwa Kaburini

50 Kulikuwa na mtu mmoja jina lake Yusufu mwenyeji wa mji wa Arimathaya, ambaye alikuwa anautazamia Ufalme wa Mungu. Yeye ali kuwa mjumbe wa Baraza na pia alikuwa mtu mwema na mwenye kuheshi mika.51 Lakini yeye hakukubaliana na wajumbe wenzake katika uamuzi wao na kitendo cha kumsulubisha Yesu.52 Basi, Yusufu alikwenda kwa Pilato akaomba apewe mwili wa Yesu.53 Akaushusha kutoka msalabani, akauzungushia sanda, akauhifadhi katika kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kaburi hilo lilikuwa halijatumika bado.54 Siku hiyo ilikuwa Ijumaa, Siku ya Maandalizi, na sabato ilikuwa karibu ianze.55 Wale wanawake waliokuwa wamefuatana na Yesu kutoka Galilaya wakamfuata Yusufu, wakaliona kaburi na jinsi mwili wa Yesu ulivyolazwa humo.56 Kisha wakarudi nyumbani wakaandaa marashi na manukato ya kuupaka huo mwili. Lakini waka pumzika siku ya sabato kama ilivyoamriwa.

Read full chapter