/home/mylanguagenet/public_html/sites/mylanguage.net.au/files/4sl/Swa4.html

Je, Umesikia Juu Ya… <b> Kanuni Nne Za Kiroho? </b>

Kila jambo maishani lina kanuni zake. Kadhalika maisha ya kiroho yana kanuni zake za jinsi ya kushirikiana na Mungu.


1. Mwenyezi Mungu anakupenda , naye amekupangia mpang o wa ajabu kwa maisha yako.

UPENDO WA MUNGU

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” (Yohana 3:16).

MPANGO WA MUNGU KWAKO

[Yesu alisema:] “Mimi nilikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” (Yohana 10:10)

Je, kwa nini watu wengi hawana uzima huo?


2. Mwanadamu ni mwenye dhambi naye amejitenga na Mungu . Kwa sababu hiyo hawezi kujua upendo wa Mungu kwake.

MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI

“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” (Warumi 3:23)

Mungu alimuumba mwanadamu kwa kusudi la kushirikiana naye, lakini mwanadamu alikwenda kinyume cha mpango wa Mungu. Alichagua kumwasi Mungu badala ya kumtii. Kumuasi Mungu ni kufanya dhambi. Mtu anapoishi kinyume cha mapenzi ya Mungu anaendelea kuishi maisha ya dhambi.

MWANADAMU AMETENGANA NA MUNGU

“Lakini maovu yenu yamewatenga ninyi na Mungu wenu.” (Isaya 59:2)

Mchoro huu unaashiria ya kwamba mwenyezi Mungu Mtakatifu hana ushirika na dhambi. Kati yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa wa dhambi. Mwanadamu hujaribu kumfikia Mungu kwa njia nyingi: dini, matendo mema, sala, n.k., lakini hizi zote hazitoshi. Mwanadamu bado ni mwenye dhambi.

Kuna njia moja tu ya kushirikiana na Mungu …


3. Yesu Kristo ndiye njia ya pekee ya kuondoa dhambi. Alikufa kwa ajili yako iliujue upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yako.

ALIKUFA ILI ATULETE KWA MUNGU

“Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu.” (1 Petro 3:18)

YESU YUHAI

“Kristo alikufa kwa ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko.” (1 Wakorintho 15:3,4)

YESU NDIYE NJIA YA PEKEE

“Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” (Yohana 14:6).

Mwanadamu peke yake hawezi kujirudisha kwa Mungu. Mungu alimtuma Yesu afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na tena awe daraja kati yetu na Mungu ili atulete kwa Mungu.

Sasa kanuni ya nne itakuambia jinsi uwezavyo kumjua maishani mwako…


4. Inakupasa kumpokea Yesu awe Mwokozi wako na Bwana wako. Ndipo utakapojua upendo na mpango wa mungu kwa maisha yako

Inakupasa kumpokea Kristo

"Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake." (Yohana 1:12)

UNAMPOKEA KRISTO KWA IMANI

"Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu." (Waefeso 2:8,9)

INAKUPASA KUMKARIBISHA YESU, MAISHANI MWAKO

Yesu asema: “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha, mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake.” (Ufunuo 3:20)

Kumpokea Yesu Kristo ni:

    Kutambua ya kuwa wewe ni mwenye dhambi na kugeuka nafsi yako kwa Mungu na kutubu.
    Kumtegemea Mungu na atakusamehe dhambi zako zote.
    Kumkaribisha Yesu Kristo atawale maisha yako kwa imani ili uwe kama anavyopenda.

KRISTO YUKO NJE YA
MAISHA YAKE

MTU AMEPOKEA KRISTO MAISHANI MWAKE

Mtu huyu anajitawala na kujiongoza mwenyewe

Kristo anamtawala na kumwongoza

Picha gani ni mfano wa maisha yako?

Unapenda picha gani kuwa mfano wa maisha yako?

Kama sala hii ni sawa na haja ya moyo wako, basi omba sasa na umkaribishe Kristo aingie maishani mwako.


UNAWEZA KUMPOKEA KRISTO SASA kwa maombi ukiamini

Mungu anaufahamu moyo wako. Yafuatayo katika sala hii yanaweza kukusaidia kumpokea Kristo ukiomba kwa moyo wa kweli.

"Bwana Yesu Kristo, ninakuhitaji, mimi ni mwenye dhambi. Nimekubali kwamba nimeyatawala maisha yangu mwenyewe, na kutengana nawe. Asante kwa kifo chako msalabani kwa ajili ya dhambi zangu na kwa kunisamehe zote. Sasa nageuka na kutubu. Bwana, nakuomba uingie ndani ya maisha yangu na kunitawala kabisa. Badili maisha yangu yawe kama upendavyo wewe. Amin."

Je, sala hii ni sawa na haja ya moyo wako?

Kama sala hii ni sawa na haja ya moyo wako, basi omba sasa na umkaribishe Kristo aingie maishani mwako.


JINSI YA kujua YESU YUMO MAISHANI MWAKO

Je, umemkaribisha Yesu maishani mwako? Unajuaje? Kwa hivyo yuko wapi sasa? Kumbuka Ufunuo 3:20. Yesu alisema ataingia katika maisha yako. Je, si kweli alivyosema? Je, unajuaje kuwa Mungu amesikia ombi lako? Mungu ameahidi kwamba lo lote tuombalo na kuamini litatendeka.

ALIYE NA YESU, ANAO UZIMA WA MILELE

“Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini jina la Mwana wa Mungu.” (Yohana 5:11-13.

Umshukuru Mungu kila siku kwamba Yesu anaishi katika maisha yako. Uwe na hakika kwamba hatakuacha kabisa (Mathayo 28:20). Amekupa uzima wa milele.


USITEGEMEE HISIA ZA MOYO WAKO.

Unaweza kujisikia leo una furaha mara kesho ukawa na huzuni. Kwa vyovyote utakavyojisikia Yesu Kristo habadiliki maishani mwako (Waebrania 13:5.)

    Ukweli wa Mungu ndio wenye uwezo wa kutuongoza.
    Tunaunganishwa na uwezo wa ukweli kwa imani.
    Tunapotii ukweli, hisia zetu huongozwa vyema.
    Tunamtegea Mungu na ukweli wake wala sio hisia zeta.

Tukifanya dhambi tunatubu na yeye anatusamehe.


KWA KUWA SASA UMEMPOKEA YESU

Tangu ulipo amua kumpokea Kristo mabadiliko mengi yametokea.

    Yesu ameingia katika maisha yako. (Ufunuo 3:20)
    Umesamehewa dhambi zako. (Wakolosai 1:14)
    Umefanyika kuwa mwana wa Mungu. (Yohana 1:12)
    Utazidi kujua makusudi ya Mungu kwa maisha yako. (2 Wakorintho 5:14,15,17)

Je, unafikiri kuna jambo lililo bora kuliko kumpokea Yesu katika maisha yako? Basi, labda ungependa kumshukuru Mungu sasa kwa vile alivyokurehemu. Tunathibitisha imani yetu tunapomshukuru Mungu kwa maombi.

Tuombe tukiwa huru.

Na sasa je?


JINSI YA KUKUA KIROHO

Kama mtoto mchanga unahitaji kukua utaendelea vizuri katika maisha ya kiroho ukiyafuata mashauri yafuatayo kila siku:

1. Zungumza na Mungu kwa maombi. (Yohana 15:7)

2. Soma Neno la Mungu. (Matendo 17:11)

3. Uwe mwaminifu kwa Mungu. (Yohana 14:21)

4. Mshuhudie Kristo kwa matendo yako na maneno yako. (Mathayo 4:19 na Yohana 15:8)

5. Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako. (1 Petro 5:7)

6. Umruhusu Roho Mtakatifu akutawale. (Wagalatia 5:16-18 na Matendo 1:8)


NI MUHIMU KWA WAKRISTO KUSHIRIKIANA

Biblia inatuambia tukusanyika pamoja (Waebrania 10:25). Hebu, tutumie mfano wa moto. Kuni nyingi zikilundikwa pamoja zinawaka vizuri sana, lakini ukiuondoa ukuni mmoja na kuuweka peke yake utapoa. Vile vile wewe haifai kuishi maisha ya kikristo peke yako. Ukishirikiana na watu wengine ambao wamempokea Yesu kuwa Mwokozi wao utazidi kuwa na moto wa imani. Uhudhurie kanisa ambamo watu wanaiamini Biblia kuwa ni kweli na Yesu anatukuzwa.


Kenya

LIFE Ministry
PO Box 62500
Nairobi, Kenya

[254] (2) 723‑153

lmkenya@maf.org

Tanzania

LIFE Ministry
PO Box 7962
Dar es Salaam, Tanzania

[255] (022) 246-1965

lifeministrytz@Acexnet.com

Uganda

LIFE Ministry
PO Box 695
Kampala Uganda

[256] (41) 231-951

asiimwe@africaonline.co.ug

Zimbabwe

Campus Crusade for Christ
P/Bag BW 6249
Borrowdale, Harare

[263] (4) 705-840

cccsea@ccc.org.zw