Discuss with your friends
Would you like to discover for yourself what God is like and how God wants you to live?
Most people like to make these discoveries in a group with their friends. Here are some questions to get your discussion started
Discovering Spiritual Community #15
Caring for one another
1. Una shukuru kwa ajili ya nini juma hili?
2. Una sumbukana na nini na jinsi gani tunaweza kukusaidia?
Accountability
3. Ni vipi uliweka kwa matendo tulio jifunza mwisho?
4. Ulishiriki na nani somo lililopita na matokeo yalikuwaje?
5. What needs did you meet in the community last week?
Discover
6. Uliza mtu asome kifungo kimoja kwa wakati.
7. Kuwa na mmoja katika kikundi na aseme kifungo kwa maneno yake mwenyewe.
8. Uliza kikundi kama amewacha au kuongeza kitu.
Yohana 11:1-44
5 Kwa hiyo ijapokuwa Yesu aliwapenda Martha, Mariamu na Lazaro,6 alipopata habari kuwa Lazaro ni mgonjwa, aliendelea kukaa huko alikokuwa kwa siku mbili zaidi.7 Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Twendeni tena Yudea.”8 Wanafunzi wake wakam wambia, “Mwalimu, utakwendaje tena Yudea ambako siku chache tu zilizopita Wayahudi walitaka kukupiga mawe?”9 Yesu akawajibu, “Si kuna masaa kumi na mawili ya mchana katika siku moja? Mtu akitembea mchana hawezi kujikwaa kwa maana kuna mwanga wa ulim wengu.10 Lakini mtu akitembea usiku hujikwaa kwa sababu hana mwanga nafsini mwake.”
11 Baada ya kusema haya Yesu aliongezea kusema, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini nakwenda kumwamsha.”
2 Wanafunzi wakamwambia, “Bwana, kama amelala bila shaka atapona.”13 Yesu alikuwa amemaanisha kuwa Lazaro amekufa, lakini wanafunzi wake hawakuelewa. Walidhani amesema Lazaro amelala usingizi.14 Kwa hiyo Yesu akawaambia wazi wazi, “Lazaro amekufa.15 Hata hivyo nafurahi sikuwepo kabla Lazaro kufa. Hii itakuwa kwa faida yenu, ili muweze kuamini. Lakini sasa twendeni.”16 Tomaso aliyeitwa Pacha akawaambia wanafunzi wenzake, “Na sisi pia twendeni tukafe pamoja naye.”
Yesu Ni Ufufuo Na Uzima
17 Yesu alipowasili alikuta Lazaro alikwisha zikwa siku nne zilizopita.18 Kwa kuwa kijiji cha Bethania kilikuwa umbali wa kama kilometa tatu tu kutoka Yerusalemu,19 Wayahudi wengi wal ikuwa wametoka mjini kuja kuwafariji Martha na Mariamu kwa kifo cha ndugu yao.20 Martha aliposikia Yesu amefika, alitoka kwenda kumpokea, ila Mariamu akabaki amekaa ndani.21 Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangali kufa.22 Na hata sasa ninafahamu kuwa cho chote utakachomwomba Mungu, atakutimizia.”23 Yesu akamwambia, “Kaka yako atakuwa hai tena.”24 Martha akamjibu, “Ndio, ninajua ya kuwa atakuwa hai tena wakati wa ufufuo, siku ya mwisho.”25 Yesu akamwambia, “Mimi ndiye ufufuo na uzima; mtu akiniamini mimi, hata akifa ataishi;26 na ye yote anayeishi akiwa ananiamini hatakufa kamwe. Je, unaamini haya?”27 Martha akajibu, “Ndio Bwana; ninaamini ya kuwa wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu, ambaye ange kuja ulimwenguni.”
Yesu Analia
28 Baada ya kusema haya Martha alikwenda akamwita Mariamu kando akamwambia, “Mwalimu amefika na anakuita.”29 Mariamu akaondoka upesi akaenda alipokuwa Yesu.30 Yesu alikuwa bado hajaingia kijijini. Alikuwa bado yuko pale Martha alipokutana naye.31 Wale Wayahudi waliokuwa wakimfariji Mariamu walipoona ameondoka haraka, walidhani anakwenda kaburini kuomboleza, kwa hiyo wakamfuata.32 Mariamu alipomwona Yesu aliinama chini kwa heshima akasema, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu han galikufa.”33 Yesu alipomwona Mariamu akilia na wale Wayahudi waliokuja naye pia wanalia, alifadhaika sana moyoni;34 akau liza, “Mmemzika wapi?” Wakamwambia, “Bwana, njoo uone.”35 Yesu akalia.36 Wale Wayahudi wakasema, “Tazameni jinsi alivyompenda Lazaro!”37 Lakini wengine wakasema, “Alimponya kipofu, kwa nini hakuweza kuzuia Lazaro asife?”
Yesu Amfufua Lazaro
38 Yesu akafika penye kaburi akiwa amefadhaika sana. Kaburi lenyewe lilikuwa katika pango ambalo mlango wake ulikuwa umezibwa kwa jiwe.39 Akasema, “Ondoeni hilo jiwe.” Dada yake mare hemu, Martha, akasema, “Bwana, patakuwa na harufu kali kwani siku nne zimepita tangu azikwe.”40 Yesu akamjibu, “Sikukuam bia kama ungeamini ungeuona utukufu wa Mungu?”41 Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe. Yesu akaangalia mbinguni akasema, “Baba ninakushukuru kwa kunisikia.42 Ninajua ya kuwa huwa unanisikia wakati wote, lakini nimesema hivi kwa faida ya hawa walio hapa, ili wapate kuamini ya kuwa umenituma.”43 Baada ya kusema haya akapaaza sauti akaita, “Lazaro, toka nje!”44 Yule aliyekuwa amekufa akatoka, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa. Yesu akawaambia, “Mfungueni awe huru!”
Copyright © 1989 by Biblica
Read More
Application
9. Ukimaliza vivungo vyote, uliza mtu katika kikundi aseme hadithi yote kwa kichwa. Wacha kikundi kirekebishe makosa.
10. Kifungo hiki kinatueleza nini kuhusu Mungu?
11. Kifungu hiki kinatueleza nini kuhusu wanadamu?
Planning
12. Kama kifungo hiki ni kweli, ni tabia ipi tunafaa kubadilisha juma hili?
13. Utamweleza nani kuhusu hadithi hii juma hili?
14. Mahitaji yapi tunaweza kuyatekeleza juma hili katika jamii?









