Discuss with your friends
Would you like to discover for yourself what God is like and how God wants you to live?
Most people like to make these discoveries in a group with their friends. Here are some questions to get your discussion started
Discovering Spiritual Community #4
Caring for one another
1. Una shukuru kwa ajili ya nini juma hili?
2. Una sumbukana na nini na jinsi gani tunaweza kukusaidia?
Accountability
3. Ni vipi uliweka kwa matendo tulio jifunza mwisho?
4. Ulishiriki na nani somo lililopita na matokeo yalikuwaje?
5. What needs did you meet in the community last week?
Discover
6. Uliza mtu asome kifungo kimoja kwa wakati.
7. Kuwa na mmoja katika kikundi na aseme kifungo kwa maneno yake mwenyewe.
8. Uliza kikundi kama amewacha au kuongeza kitu.
Mwanzo 22:1-19
2 Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.
3 Ibrahimu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.
4 Siku ya tatu Ibrahimu akainua macho yake, akapaona mahali pakali mbali.
5 Ibrahimu akawaambia vijana wake, Kaeni ninyi hapa pamoja na punda, na mimi na kijana tutakwenda kule, tukaabudu, na kuwarudia tena.
6 Basi Ibrahimu akazitwaa kuni za hiyo sadaka, akamtwika Isaka mwanawe; akatwaa moto na kisu mkononi mwake, wakaenda wote wawili pamoja.
7 Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa?
8 Ibrahimu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu. Basi wakaendelea wote wawili pamoja.
9 Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni.
10 Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe.
11 Ndipo malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.
12 Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.
13 Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.
14 Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire,kama watu wasemavyo hata leo,Katika mlima wa BWANA itapatikana.
15 Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni
16 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,
17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;
18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.
19 Basi Ibrahimu akawarudia vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja mpaka Beer-sheba; Ibrahimu akakaa huko Beer-sheba.
Read More
Application
9. Ukimaliza vivungo vyote, uliza mtu katika kikundi aseme hadithi yote kwa kichwa. Wacha kikundi kirekebishe makosa.
10. Kifungo hiki kinatueleza nini kuhusu Mungu?
11. Kifungu hiki kinatueleza nini kuhusu wanadamu?
Planning
12. Kama kifungo hiki ni kweli, ni tabia ipi tunafaa kubadilisha juma hili?
13. Utamweleza nani kuhusu hadithi hii juma hili?
14. Mahitaji yapi tunaweza kuyatekeleza juma hili katika jamii?









