Read God's Word: the Bible
- What does this tell you about God?
- What does this tell you about Jesus?
- What does this tell you about people?
- If this is true, what difference would it make in your life?
- Who are five people who you can share your discoveries with?
Luka 19
Mfano Wa Fedha
11 Wakati walipokuwa wanasikiliza haya, Yesu aliendelea kuwaambia mfano. Wakati huo watu walikuwa wakidhani kwamba kwa kuwa walikuwa wanakaribia Yerusalemu, Ufalme wa Mungu ungetokea mara.12 Kwa hiyo akawaambia: “Mtu mmoja wa ukoo wa kitawala, alisafiri kwenda nchi ya mbali ili akapokee madaraka ya kuwa mfalme, kisha arudi.13 Akawaita watumishi wake kumi akawapa kila mmoja fungu la fedha. Akawaambia, ‘Zitumieni kufanyia biash ara mpaka nitakaporudi.’14 Lakini raia wake walimchukia wakapeleka ujumbe usemao, ‘Hatutaki huyu mtu awe mfalme wetu. ’15 Hata hivyo alipewa ufalme akarudi nyumbani. Kisha akawaita wale watumishi aliokuwa amewaachia fedha, ili afahamu faida kila mmoja wao aliyopata.
16 “Wa kwanza akaja, akasema, ‘Bwana, kutokana na fedha uliyoniachia nimepata faida mara kumi zaidi.’17 Yule bwana akamjibu, ‘Umefanya vizuri mtumishi mwema! Kwa sababu umekuwa mwaminifu katika wajibu mdogo sana, nakupa mamlaka juu ya miji kumi.’
18 “Wa pili naye akaja, akasema, ‘Bwana, fedha yako imeleta faida mara tano zaidi.’19 Bwana wake akajibu, ‘Nakupa mamlaka juu ya miji mitano.’20 Kisha akaja mtumishi mwingine akasema, ‘Bwana hii hapa fedha yako. Niliitunza vizuri kwenye kitambaa.21 Nilikuogopa, kwa sababu wewe ni mtu mkali. Unachukua ambapo hukuweka kitu na unavuna mahali ambapo hukupanda kitu.’
22 “Bwana wake akamjibu, ‘Nitakuhukumu kwa maneno yako mwe nyewe, wewe mtumishi mwovu ! Kama ulifahamu kwamba mimi ni mtu mkali, nichukuaye mahali ambapo sikuweka kitu na kuvuna ambapo sikupanda;23 kwa nini basi hukuweka fedha zangu benki ili nita kaporudi nizichukue na faida yake?’24 Ndipo akawaambia wale waliokuwa wamesimama karibu , ‘Mnyang’anyeni fungu lake la fedha mkampe yule mwenye kumi.’25 Wakamwambia, ‘Bwana, mbona tayari anayo mafungu kumi’?26 Akajibu, ‘Nawahakikishieni kwamba, kila aliye na kitu, Mungu atamwongezea; na yule asiyetumia alicho nacho, atanyang’anywa hata hicho alicho nacho.27 Sasa nileteeni wale maadui zangu ambao hawakutaka mimi niwe mfalme wao; waleteni hapa muwaue mbele yangu.”’
Yesu Aingia Yerusalemu
28 Alipokwisha kusema haya, Yesu alikaa mbele ya msafara akielekea Yerusalemu.29 Na alipokaribia Bethfage na Bethania kwenye mlima wa Mizeituni aliwatuma wanafunzi wawili akawaagiza hivi,30 “Nendeni katika kijiji kile kilicho mbele yenu. Mtaka pokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana-punda ambaye hajapandwa na mtu bado, amefungwa. Mfungueni, mumlete hapa.31 Kama mtu akiwauliza, ‘Mbona mnamfungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji.”’
32 Wale waliotumwa wakaenda, wakakuta kila kitu kama Yesu alivyokuwa amewaambia.33 Walipokuwa wanamfungua yule mwana- punda wenyewe wakawauliza, “Mbona mnamfungua huyo mwana-punda?”34 Wale wanafunzi wakajibu, “Bwana anamhitaji.”35 Wakamleta kwa Yesu. Wakatandika mavazi yao juu ya huyo mwana-punda, kisha wakampandisha Yesu juu yake.36 Alipokuwa akienda, watu wakatan daza nguo zao barabarani.37 Alipokaribia mteremko wa mlima wa Mizeituni, umati wote wa wanafunzi wake wakaanza kwa sauti kuu kumsifu Mungu kwa furaha kwa ajili ya miujiza yote waliyoiona Yesu akifanya,38 wakasema: “Amebarikiwa Mfalme anayekuja kwa jina la Bwana! Amani mbinguni na Utukufu kwa Mungu.”39 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwemo katika umati wakamwambia, “Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako.”40 Yesu akawajibu, “Nawaambia, hawa wakinyamaza, mawe yatapiga kelele.”
Yesu Anaulilia Mji Wa Yerusalemu
41 Alipokaribia Yerusalemu, akauona mji, aliulilia,
42 akasema, “Laiti ungalijua leo jinsi ya kupata amani! Lakini sasa huoni!43 Kuna siku ambapo maadui zako watakuzungushia ukuta na kukuzingira na kukushambulia kutoka kila upande.44 Watakutupa chini wewe na wanao ndani ya kuta zako na hawataacha hata jiwe moja juu ya jingine. Hii ni kwa sababu hukutaka kutambua wakati
Yesu Aingia Hekaluni
45 Ndipo akaingia Hekaluni akaanza kuwafukuza wale wal iokuwa wakifanya biashara humo.46 Akawaambia, “Imeandikwa katika Maandiko, ‘Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala.’ Lakini ninyi mmeigeuza kuwa pango la wanyang’anyi.”
47 Kila siku alikuwa akifundisha Hekaluni. Makuhani wakuu na walimu wa sheria wakiungwa mkono na viongozi wengine walijaribu kila njia wapate kumwua48 lakini hawakupata nafasi kwa sababu watu wote waliomfuata waliyasikiliza maneno yake kwa makini na kuyazingatia. Yesu Aulizwa Kuhusu Mamlaka Yake
Copyright © 1989 by Biblica
Read More









