Read God's Word: the Bible
- What does this tell you about God?
- What does this tell you about Jesus?
- What does this tell you about people?
- If this is true, what difference would it make in your life?
- Who are five people who you can share your discoveries with?
Luka 11
Yesu Na Beelzebuli
14 Yesu alikuwa anamtoa pepo mtu mmoja ambaye alikuwa bubu. Pepo huyo alipotoka, yule mtu akaanza kusema! Watu wakashangaa.15 Lakini wengine wakasema: “Anatoa pepo kwa uwezo wa Beelzeb uli, yule mkuu wa pepo wote.”16 Wengine wakamjaribu kwa kum womba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.
17 Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, “Nchi yo yote iliyo na mgawanyiko wa vikundi-vikundi vinavyopingana au familia yenye mafarakano, huangamia.18 Kama ufalme wa shetani ungekuwa umega wanyika wenyewe kwa wenyewe ungesimamaje? Nasema hivi kwa sababu mnasema ninaondoa pepo kwa uwezo wa Beelzebuli.19 Kama mimi ninaondoa pepo kwa nguvu za Beelzebuli, wafuasi wenu je, wao huwaondoa pepo kwa uwezo wa nani? Wao watawaamulia.20 Lakini kwa kuwa ninaondoa pepo kwa uwezo wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umewajia.21 Mtu mwenye nguvu aliye na silaha anapoilinda nyumba yake, mali yake ni salama.22 Lakini mtu mwenye nguvu zaidi akimshambulia na kumshinda, atamnyang’anya silaha alizozitegemea na kugawanya mali yote.23 “Mtu ambaye hayuko upande wangu, anapingana nami, na mtu asiyekusanya pamoja nami, anatawanya.
24 “Pepo mchafu akimtoka mtu, anazunguka jangwani akitafuta mahali pa kupumzikia. Asipopata anasema, ‘Kwa nini nisirudi kwe nye nyumba yangu niliyotoka?’25 Akirudi, na kuikuta ile nyumba ni safi na imepangwa vizuri,26 huenda kuwaleta pepo wengine saba wachafu kuliko yeye wakaingia na kuishi humo. Na hali ya sasa ya mtu huyo inakuwa mbaya kuliko ya kwanza.”
27 Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika umati akasema kwa nguvu, “ Amebarikiwa mama aliyekuzaa na kukunyon yesha.”28 Yesu akajibu, “Wamebarikiwa zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kulifuata.”
Ishara Ya Yona
29 Umati wa watu ulipozidi kuongezeka, Yesu aliendelea kufundisha akisema, “Watu wa kizazi hiki ni waovu. Wanatafuta ishara lakini hawatapewa ishara yo yote isipokuwa ile ya nabii Yona.30 Kwa maana kama Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninawi, ndivyo mimi Mwana wa Adamu nitakavyokuwa ishara kwa kizazi cha sasa.31 Siku ya hukumu malkia wa Sheba atashuhudia kwamba watu wa sasa wana hatia kwa sababu yeye alisafiri kutoka mbali kuja kusikiliza hekima ya Sulemani. Lakini sasa, aliye mkuu kuliko Sulemani yuko hapa.32 Siku ile ya hukumu, watu wa Ninawi watashuhudia kwamba watu wa sasa wana hatia kwa sababu Yona ali powahubiria waliacha dhambi zao. Lakini sasa aliye mkuu kuliko
Taa Ya Mwili
33 “Hakuna mtu awashaye taa akaificha au kuifunika, ila huiweka mahali pa juu ili watu wote wanaoingia waone nuru yake.34 Jicho lako ni nuru ya mwili wako. Macho yakiwa mazima huan gaza mwili wako wote; lakini yakiwa mabovu, mwili wako pia uta kuwa katika giza.35 Kwa hiyo hakikisha kwamba una nuru ndani yako, wala si giza.36 Ikiwa mwili wako wote una nuru, bila sehemu yo yote kuwa gizani, basi utang’aa kabisa kama inavyokuwa wakati taa inapokuangazia.”
Yesu Awaonya Mafarisayo Na Wanasheria
37 Yesu alipomaliza kuzungumza, Farisayo mmoja alimkaribisha nyumbani kwake kwa chakula. Yesu akaingia na kuketi chakulani moja kwa moja.38 Farisayo yule alipoona kwamba Yesu hakunawa kwanza kabla ya kula alishangaa.39 Ndipo Bwana akamwambia, “Ninyi Mafarisayo mnasafisha kikombe na sahani kwa nje huku ndani mmejaa udhalimu na uovu.40 Wajinga Ninyi! Hamjui kuwa yeye aliyetengeneza sehemu ya nje ndiye aliyetengeneza na ya ndani pia?41 Watendeeni ukarimu maskini kwa kuwapa vilivyomo ndani ya vikombe na sahani zenu na kila kitu kitakuwa safi kwenu.
42 “Lakini ole wenu, Mafarisayo! Ninyi mnamtolea Mungu sehemu ya kumi ya mnanaa, mchicha na kila aina ya mboga lakini mnapuuza haki na kumpenda Mungu. Mngeweza kutoa matoleo hayo pasipo kusahau haki na upendo kwa Mungu.
43 “Ole wenu, Mafarisayo! Ninyi mnapenda kuketi viti vya mbele katika masinagogi na kusalimiwa kwa heshima masokoni!44 Ole wenu! Kwa maana ninyi ni kama makaburi yasiyokuwa na alama, ambayo watu huyakanyaga pasipo kujua.”
45 Mwalimu mmoja wa sheria akasema, “Mwalimu, unapozungumza hivyo unatushutumu na sisi wanasheria!”46 Yesu akamjibu, “Hata ninyi wanasheria, ole wenu! Mnawabebesha watu mzigo wa sheria ambazo hawawezi kuzitimiza; wala hamfanyi lo lote kuwa saidia iwe rahisi kwao kuzitimiza.47 Ole wenu kwa kuwa mnawa jengea makaburi manabii waliouawa na babu zenu.48 Kwa kufanya hivyo mnakiri kwamba mnaunga mkono kitendo hicho walichofanya babu zenu. Wao waliua na ninyi mnatengeneza makaburi.
49 “Ndio maana Mungu katika hekima yake alisema, ‘Nita wapeleka manabii na mitume, na baadhi yao watawaua na wengine watawatesa.’50 Kwa hiyo damu ya manabii wote iliyomwagika tangu mwanzo wa dunia itahesabiwa juu ya watu wa kizazi hiki;51 tangu damu ya Abeli mpaka damu ya Zakaria aliyeuawa kati ya madhabahu na mahali patakatifu. Nawaambia kweli, watu wa kizazi hiki wataadhibiwa kwa ajili yao wote.52 Ole wenu ninyi wanashe ria kwa maana mmeuchukua ufunguo unaofungua nyumba ya maarifa. Ninyi wenyewe hamkuingia na wale waliokuwa wanaingia mkawazuia.”
53 Yesu alipoondoka hapo, walimu wa sheria na Mafarisayo wakawa wanampinga vikali na kumwuliza maswali mengi,54 wakijar ibu kumtega ili aseme kitu ambacho watakitumia kumshitaki.
Copyright © 1989 by Biblica
Read More









